Posts

HISIA ZA MOYO WANGU             1.          Nilikuona u kinda, mpaka leo nakuona,                         Unaenda kwa kupinda, na kusimama hakuna,                         Japo me nilikupenda,hilo wewe hukuona,                         Sasa leo nimeona, niseme bila kupinda. 2.          Niseme bila kupinda, hilo jambo la moyoni,             Niseme ninakupenda, sasa siyo utotoni,             Wewe sasa siyo kinda, nasema bila utani,             Wewe ndo nimekupenda, sasa na wewe pendeka. 3.          Sasa nawe pendeka, ujana maji ya moto,             Kwa kalamu naandika, na si jambo la kitoto,             Nimejitoa sadaka, kuzama ndani ya mto,             Mapenzi ni kama maji, ukinywa kiu yaisha. 4.          Ukinywa kiu yaisha, ndo raha ya hilo penzi,             Bunduki yaweza isha ,hilo unajua mwenzi,             Hata risasi kuisha,nikitaka lako penzi,             Ninalewa lako penzi, na uwe wangu azizi. 5.          Na uwe wangu azizi, si kwamba